22 Desemba 2024 - 16:01
Waziri Mkuu wa Uhispania ametaka kutambuliwa rasmi kwa "Palestina"

Waziri Mkuu wa Uhispania kwa mara nyingine ametoa wito wa kutambuliwa rasmi "Palestina" kama nchi huru.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Waziri Mkuu wa Uhispania "Pedro Sanchez" kwa mara nyingine tena amezitaka nchi za Dunia kuitambua rasmi Palestina kama nchi huru.

Alisema maneno hayo katika mkutano wa "Ujamaa wa Kimataifa" uliofanyika katika Mji Mkuu wa Morocco.

Sanchez alisisitiza: Ukaliaji wa Israel (kwa Palestina) lazima ukomeshwe na kuruhusu watu wa Palestina waanzishe Taifa lao Huru, na Jerusalem Mashariki kuwa Mji Mkuu wake ndani ya mfumo wa suluhisho la Serikali mbili.

Aidha amesisitiza ulazima wa kukomesha vikwazo na matatizo ya kibinadamu ya Wapalestina na kutoa wito wa kuwepo ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na migogoro hiyo.

Mwezi uliopita, Uhispania ililitambua rasmi Taifa la Palestina na kuchukulia hatua hii kuwa inalingana na maazimio ya Umoja wa Mataifa na hatua ya kufikia amani.