Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamepiga nara za kulaani hatua ya serikali ya Ufaransa ya kuendelea kutoa himaya na uungaji mkono kwa utawala haramu wa Israel unaofanya mauaji ya umati katika Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao pia wameitaka serikali ya Ufaransa kutekeleza hati ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Waziri wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant na kuwaka vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia dhidi ya Israel.
Katika majuma ya hivi karibuni maelfu ya wafuasi wa wananchi wa Palestina wamekuwa wakifanya maandamano katika miji mingi muhimu duniani ikiwemo Paris, Berlin, Santiago, Amsterdam, Copenhagen, Istanbul, Rome, Manchester na London kulaani mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na Lebanon.
Hivi karibuni mashabiki wa timu ya Maccabi Tel Aviv walizusha fujo na machafuko nchini Uholanzi kwa kuwashambulia waungaji mkono wa Palestina na kuwachokoza kabla na wakati wa mechi ya soka ya Ligi ya Ulaya UEFA kati ya timu hiyo ya Kizayuni na Ajax Amsterdam ya Uholanzi.
parstoday