24 Desemba 2024 - 13:23
Ripoti ya Picha |  Hafla ya kuzaliwa kwa Sayyidat Fatima (s.a) na kuzaliwa kwa Hadhrat Issa -Yesu- (a.s) katika Jiji kubwa zaidi la Ivory Coast

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA- Kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Sayyidat Fatima (s.a) na kuzaliwa kwa Hadhrat Issa -Yesu- (a.s), limefanyika Tamasha kubwa lililopewa jina la: "Amani, Upendo na Udugu" lililoandaliwa na Jumuiya ya Al-Ghadir ya Ivory Coast kwa ushirikiano na Kituo cha Kikristo cha: "Maombi ya "Amani". Tamasha hilo lilifanyika katika Jiji la Abidjan, ambapo mamia ya watoto kutoka Ivory Coast na Lebanon walishiriki katika Tamasha hilo.