26 Desemba 2024 - 17:11
Mashia 200 walikamatwa na Polisi wa Nigeria

Polisi wa Nigeria waliwakamata Mashia 200 wakiwemo Wanawake na Watoto katika Mji wa Abuja.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul Bayt (a.s) - ABNA - Polisi wa Nigeria waliwakamata idadi kubwa ya Mashia, akiwemo mama na mtoto wake mchanga wa miezi mitatu, kwa kushiriki katika sherehe za kidini wakati wa kuzaliwa kwa Hazrat Zahra (s.a ) huko Abuja, Mji Mkuu wa Nigeria.

Magazeti ya humu nchini yamemnukuu msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria akisema:

Ukamataji watu hao ulifanywa bila ya uhalali wowote wa kisheria, hivyo basi, wafungwa hao walikuwa wakijiandaa kumalizia sherehe hizo (za Kuzaliwa kwa Sayyidat Fatima Zahra Amani iwe juu yake) na kujiandaa kurejea majumbani mwao.Ghafla vikosi vya usalama viliingia na kuwavamia kwa nguvu.

Msemaji wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesisitiza kuwa: Wengi wa wafungwa hao walikuwa Wanawake na vijana akiwemo mtoto mchanga wa miezi mitatu. Tukio hili ni moja ya matukio ya hivi karibuni katika mfululizo wa matukio sawa na hayo ambapo vikosi vya usalama vililenga raia, kutumia vibaya mamlaka yao, na kukiuka haki za kisheria, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kukusanyika kwa amani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashahidi hao, idadi ya waliokamatwa ilikuwa karibia watu 200.

Tukio hili lilizua hali ya kutofurahishwa na kutoridhika kwa vuguvugu la Kidini na Kisiasa na Mashirika ya Haki za Binadamu nchini Nigeria, ambayo yalitaka uchunguzi wa wahusika wa kukamatwa kidhulma kwa watu hao.