28 Desemba 2024 - 19:53
Katika tukio la kuzaliwa kwa Masih (Yesu), Kibanda cha Sayansi ya Mwokozi kilianzishwa / kilijengwa nchini Uswidi + Picha

Katika hafla ya kuzaliwa Yesu Kristo / Masih Issa bin Maryam (Amani iwe juu yake) vijana wa kampeni ya "Ni nani Imam Mahdi" walianzisha / walijenga Kibanda cha "Mjue Mwokozi" nchini Sweden (Uswidi).

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Kampeni ya "Ni nani Imam Mahdi (amani iwe juu yake)?", ni kampeni ya Kimataifa ambayo kwa sasa inafanya kazi kwa lugha tatu ili kumtambulisha ipasavyo Imam Mahdi (amani iwe juu yake) kwa Ulimwengu mzima katika nchi tofauti tofauti. Kauli mbiu ya kampeni hii ni; "Hebu tumjue kwa usahihi Imam Mahdi (amani iwe juu yake) na tumtambulishe kwa Ulimwengu".

Kuzaliwa kwa Masih (Yesu Kristo) ni fursa nzuri kwa watu wa nchi za Ulaya, ambao wengi wao ni Wakristo, kumfahamu mwokozi wa Wanadamu.