Vuguvugu hili la maandamano, ambalo lilifanyika Ijumaa ya mwisho ya 2024, lilionekana huku Bendera za Palestina zikiwa zimeinuliwa juu kutoka kwenye madirisha ya nyumba nyingi katika moja ya Barabara kuu za Mji wa Brighton.
Watetezi wa Palestina ambao tangu kuanza kwa vita huko Ghaza wameonyesha hasira na vipingamizi vyao dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni kwa kufanya maandamano katika miji tofauti ya Uingereza, safari hii walijaribu kupaza sauti zao za kupinga kitendo cha serikali hiyo kutojali hali mbaya na kuleta maafa ya kibinadamu na mauaji ya kimbari huko Gaza, kupitia njia ya mfano (kwa kuonyesha upingaji wao kivitendo na kiishara).
Serikali ya Uingereza bado haijataja jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza kuwa ni mauaji ya kimbari.