Uvamizi huo ulifanyika siku ya Jumanne, saa chache tu baada ya mashambulizi ya anga ya Israel karibu na jiji la pwani la Tartus, upande wa kaskazini wa nchi hiyo ya Kiarabu.
Vikosi vamizi vya Israel vilisonga mbele katika maeneo kadhaa ndani ya mikoa hiyo kwa msaada wa kutua kwa helikopta na misafara ya kivita ya magari ya deraya.
Shambulio hilo lilijikita hasa katika eneo la Tel al-Mal huko Dara’a na mji wa al-Mashara katika Quneitra. Vyanzo vya ndani vimeripoti kuwa vikosi vya Israel viliingia kwenye kituo cha kijeshi cha Tel al-Mal, kilicho katika viunga vya mji mkuu wa mkoa wa Quneitra, ambapo walifanya upekuzi kabla ya kuondoka.
Waangalizi wamesema kuwa matukio haya yamefanya vikosi vya utawala wa Israel kusonga mbele zaidi ndani ya Syria kuliko wakati wowote tangu mwaka 1967, wakati utawala huo ulipoikalia kwa mabavu Milima ya Golan ya Syria.
Uvamizi huo umepitiliza hata mashambulizi makali ya Israel yaliyoanza Novemba 2024 hadi sasa dhidi ya Syria, ambapo waasi wanaoungwa mkono na mataifa ya kigeni waliIangusha serikali ya kidemokrasia ya nchi hiyo.
Kabla ya uvamizi huo, ndege za kivita za Israel zilifanya mashambulizi ya anga, zikilenga kikosi cha ulinzi wa anga cha Syria karibu na Tartus.
Chombo cha habari cha utawala mpya wa Syria kilithibitisha mashambulizi hayo, kikibainisha kuwa ingawa uharibifu wa mali umetokea, hakuna vifo vilivyoripotiwa.
Jeshi la Israel lilidai kuwa mashambulizi hayo yalilenga kuzuia silaha zisiangukie mikononi mwa “maadui.”
342/
Your Comment