Katika barua ya umma iliyotolewa jana Alkhamisi, Chama cha Uongozi wa Wanafunzi (SGA) cha Kitivo cha Barnard kimeshutumu uongozi wa chuo kwa kuvunja ahadi ya muda mrefu iliyotolewa na Rais wa chuo hicho, ikisisitiza kwamba taasisi hiyo iliahidi 'kutoalika' Idara ya Polisi ya New York (NYPD) kwenye chuo kikuu.
SGA imeshiriia picha na video za kuhuzunisha za wanafunzi wenzao "wakitendewa ukatili na kunyamazishwa" walipokuwa wakishiriki maandamano ya amani, hasa kulaani uwepo wa polisi wa NYPD chuoni hapo.
Jumatano alasiri, mafisa wa polisi wa New York walihamisha wanachuo kutoka maktaba ya Chuo cha Barnard, ambapo waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina walikuwa wameketi, kulalamikia kufukuzwa kwa wanafunzi watatu wanaounga mkono Palestina, kwa madai ya tishio la bomu.
Ikumbukwe kuwa, Aprili mwaka jana, wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Columbia nchini Marekani walianzisha maandamano ya kupinga jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Palestina; maandamano yaliyochochea cheche za mwamko katika vyuo vikuu vingine vya nchi hiyo na hata katika nchi za Ulaya, licha ya mbinyo wa polisi.
Haya yanajiri huku Rais Donald Trump wa Marekani akitishia kusitisha ufadhili wa serikali kwa Vyuo Vikuu au taasisi zozote za elimu zinazoruhusu “maandamano haramu” kufanyika, akisema atachukua hatua kali dhidi ya wanachuo wanaoshiriki maandamano hayo.
Ingawa hakutaja moja kwa moja maandamano ya wanaounga mkono Palestina, Trump hapo awali alitishia kuwafukuza Marekani wanafunzi wanaoshiriki maandamano dhidi ya Israel na wanaopinga mauaji ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
342/
Your Comment