Hujjatul-Islam Mohammad Mehdi Imanipour, ameyasema hayo katika kongamano la tatu la Qur'ani la Tehran, ambapo sambamba na kuashiria miongozo ya Qur'ani kwa ajili ya kupatikana Umma Mmoja wa Kiislamu amesema: "kwa mtazamo wa Qur'ani Tukufu, kuwepo kwa Umma mmoja ni lengo la kidini, ambalo inapasa lifikiwe kwa Waislamu kupiga hatua kuelekea kwenye lengo hilo".
Mkuu wa Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran amegusia pia umuhimu wa udugu wa kidini katika kujenga Umma Mmoja na akaongeza kuwa: inapasa Umma Mmoja uimarishe moyo wa udugu. Udugu huo wa kidini inapasa uonekane katika nyanja zote za binafsi na kijamii za Waislamu.
Kongamano la tatu la Qur'ani la Tehran limefanyika hapa mjini Tehran kwa lengo la kuasisi Baraza la Qur'ani la Ulimwengu wa Kiislamu ili kutekeleza mkakati madhubuti na athirifu wa kupatikana Umma Mmoja wa Waislamu.
Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu la Iran limehudhuriwa na wanaharakati zaidi ya 50 wa Qur'ani kutoka nchi 24 duniani.
Wasomi wa masuala ya Qur'ani walioshiriki kwenye kongamano la Tatu la Qur'ani la Tehran wametoka Iran, Afghanistan, Algeria, Muungano wa Falme za Kiarabu, Indonesia, Uganda, Italia, Bosnia na Herzegovina, Pakistan, Tajikistan, Thailand, Uturuki, Chad, China, Russia, Ivory Coast, Iraq, Qatar, Cambodia, Guinea, Lebanon, Nigeria, na India.../
342/
Your Comment