13 Machi 2025 - 18:00
Wakati wa Mkutano wa Mkuu wa Mtandao wa Wilayat na Ayatollah Arafi, ilitajwa;Mtandao wa Wilayat; ni Hawza ya Mtandaoni yenye upeo wa Kimataifa na mbin

Mkuu wa mitandao ya kimataifa ya Wilayat, Hojjat-ul-Islam Sayyid Jaafar Alavi, akiwa katika mkutano na Ayatollah Arafi, Mkurugenzi wa Seminari (Hawza) nchini (Iran) alielezea shughuli, harakati na vipengele vya Mtandao huu wa Media.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) - Abna - Hojjat-ul-Islam wal-Muslimin, Sayyid Jaafar Alavi, Mkuu wa mitandao ya Kimataifa ya Wilayat, katika kikao na Ayatollah Arafi, Mkurugenzi wa seminari zote nchini Iran, ameelezea shughuli, harakati na  matendo ya Taasisi ya Kimataifa ya Wilayat na kusema: Mtandao wa Wilayat ni mtandao wenye utambulisho wa Seminari (Hawza) kabisa, na ni mtandao pekee ambao umefungwa kutoka sakafu hadi dari katika viwango tofauti vya Seminari (Hawza).

Sawa sawa iwe ni katika uwanja wa utungaji sera, mkakati, uongozi na upangaji (Mwanzilishi, Wadhamini, Baraza na Vikundi vya Kisayansi), au iwe katika uwanja wa utekelezaji na uendeshaji (Chombo cha Wanafunzi wa Vyombo vya Habari) au katika uwanja wa athari na hadhira; kwa maana kwamba, watazamaji wake wote wanavutiwa na maarifa ya kidini.

Akaongeza kusema: “Mtandao wa Wilayat kwa hakika ni Hawza ya Vyombo vya Habari na inaoenea katika Mabara matano, na tunaposema “ni Seminari (Hawza) kabisa” ina maana kwamba vipengele na pande zake zote, kuanzia mabaraza, nyadhifa na makao makuu, na hata wasikilizaji wote, ima ni watu wa elimu na maarifa au ni watafutaji wa elimu na maarifa.

Mkuu wa mitandao ya kimataifa ya Wilayat alitaja uwepo wa tabaka nyingi na tofauti za usimamizi kama moja ya sifa zingine za Shirika hili lenye nguvu la Media na akaelezea: Katika Shirika hili (la Media la Wilayat), kuna muundo thabiti na unaotumia mchakato wa Kisayansi na uhandisi kabisa, pasina kuwepo mwelekeo wa mtu binafsi, kiujumla ni muundo unaoendeshwa kwa mujibu wa hekima ya pamoja na usimamizi wa pamoja, na udhibiti maalum, uakifishaji wa michakato ya ufuatiliaji wakati wa mchakato wa uzalishaji na usambazaji, umepunguza sana kiwango cha makosa.

Mkuu wa Taasisi ya Wilayat, alipokuwa akieleza sifa za mitandao mingine ya taasisi hii, alisema: Sifa nyingine ya mitandao tofauti ya Wilayat ni umoja katika wingi uleule; kwa maana kudumisha uhuru wa utambulisho wa kila lugha na kila mtandao, kwa mujibu wa mahitaji ya hadhira, madhumuni ya eneo hilo na mahitaji yake mahususi ya kuonwa, umbo na maudhui na ladha (mahsusi ya eneo husika), huku ikidumishwa dhamira kuu katika uwanja wa kuchapisha na kusambaza mafundisho ya Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao) katika harakati kiujumla.

Aliendelea kusema kuwa: Shughuli za Taasisi ya Ulimwengu ya Wilayat ni mfano wa Hadithi isemayo:  “ «قلیلُ المؤونةِ وکثیر المَعونةِ» | Gharama kidogo na msaada (ugavi) mwingi” na akasema: Uzalishaji wote wa ndani wa Taasisi hii unafanywa kwa gharama inayokaribiana sawa na bure, jambo ambalo linaweza kuwa sio rahisi kwa mtu kuamini. Tunafanya uzalishaji wa programu mbalimbali kwa ajili ya watoto na vijana, Documentary, wataalam na programu za maingiliano ya kimaisha, uzalishaji wa programu zaidi ya mia tatu na hamsini kwa mwezi tena kwa gharama ya chini sana; na kwa baraka (ya Mwenyezi), hizi sio harakati ndogo.

Akizungumzia faida na nguvu za vyombo vya habari vya mtandao wa kimataifa wa Wilayat, alisema: Baada ya utafiti wa sayansi ya mtandao, ambao ni utafiti wa maudhui, ni kwamba mtandao wa Wilayat una nguvu zake za fomu na vivutio vya vyombo vya habari, ambapo nitataja sehemu hii baadhi ya matukio. Kwanza kabisa, programu za mtandao wa Wilayat ambazo ni Mubashara, ni ni za hakika na zinaingiliana kikamilifu, na simu (za wasikilizaji na watazamaji) zimefunguliwa bila vikwazo katika programu zote.

Mkuu wa mitandao ya kimataifa ya Wilayat alizingatia wembamba wa mstari mwekundu, kuwa changamoto, mtazamo wa uchunguzi na wa kisasa kati ya sifa za mtandao wa Wilayat na akasema: Mtandao wa Welayat ni wa kipekee katika kujibu Shubuhati (Mashaka) mbalimbali; Kutokana na ukweli huu kwamba mitandao mingi ya Shia na Maarifa, kimsingi inajihusisha tu kuadhimisha Shiari (Alama) na kuhuisha Minasaba mbalimbali, kama vile kufuatilia tu minasaba ya Maulid na Vifo, na kufanya kazi tu kwa ajili ya kundi la kimadhehebu lenye nguvu na itikadi katika mambo ya msingi; lakini, sehemu ambayo inafuatilia na kuchunguza mtiririko wa vyombo vya habari vya Wasioamini Mungu, Wakristo, Mawahabi, irafani mpya zinazoibuka na kujitokeza, mashaka (Shubuhati) za kisiasa na kiserikali, n.k., na kuchambua na kutathmini kisayansi mahitaji ya makundi hatarishi, na kupanga na kuendeleza programu, ndilo kundi la kipekee lenye baraka la Wilayat.

Your Comment

You are replying to: .
captcha