13 Machi 2025 - 17:31
Source: Parstoday
"Mshtuko" wa hali ya hewa waikumba miji mikubwa duniani, imo miji mikuu ya Afrika

Utafiti mpya wa hali ya hewa unaonyesha kuwa mabadiliko ya tabianchi tayari yanaathiri miji mingi mikubwa duniani, na kusababisha mabadiliko ya kushangaza kati ya hali ya hewa ya mvua na ya unyevu na ile ya ukame uliokithiri huku hali ya hewa ikizidi kuwa mbaya.

Utafiti huo umechambua miji 100 yenye watu wengi zaidi, pamoja na miji 12 iliyochaguliwa, na kugundua kuwa 95% ya miji hiyo ilionyesha mwelekeo wazi wa hali ya hewa ya mvua au ukame mkali.

Kwa mfano tu, mamia ya miji, ikiwa ni pamoja na Lucknow nchini India, mji mkuu wa Uhispania, Madrid, na mji mkuu wa Saudia, Riyadh, imepatwa na mabadiliko ya hali ya hewa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, na kuhama kutoka ukame uliokithiri hadi unyevu mwingi, au kinyume chake.

Mabadiliko ya hali ya hewa katika miji yanaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa raia, kuzidisha mafuriko na ukame, kutatiza upatikanaji wa maji safi, usafi wa mazingira, na chakula, kulazimisha jamii kuhama na kueneza magonjwa.

Miji mingi tayari ilikuwa ikisumbuliwa na miundombinu duni ya maji, kama vile Karachi, Pakistan, na mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Utafiti unaonyesha kuwa miji ya Hangzhou nchini Uchina, Jakarta Indonesia, na Dallas huko Texas imekumbwa na mabadiliko makubwa zaidi ya tabianchi. Miji mingine ni pamoja na Baghdad, Bangkok, Melbourne na Nairobi nchini Kenya. Mingi mingine iiiyoathiriwa sana na mabadiliko na hali ya hewa ni Cairo, Paris, Los Angeles, Cape Town (Afrika Kusini), Rio de Janeiro, Nagoya nchini Japan, Lusaka nchini Zambia, na Guangzhou nchini China.

Mvua kubwa inaweza kusababisha mafuriko, kuharibu nyumba na barabara, na kueneza magonjwa hatari yanayosababishwa na maji machafu, kama kipindupindu, haswa wakati mifumo ya maji taka inapozidiwa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha