Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -: Vyanzo vya Habari vimetangaza kuwa magaidi kutoka nchi 20 za dunia wako katika muundo mpya wa usalama wa utawala wa Kigaidi wa al-Jolani huko Syria; Kitendo ambacho hakijawahi kuonekana katika nchi yoyote ya Kiislamu au Kiarabu.
Vyanzo hivi vya habari vimeongeza kuwa: Muundo wa usalama wa Syria unajumuisha magaidi kutoka mataifa 20 tofauti, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa. Muundo huu wa usalama umekuwa kitengo cha usalama cha utawala wa kigaidi wa al-Jolani.
Makundi haya ya kigaidi yanatoka katika nchi kama vile Jamhuri ya Azerbaijan, Chechnya, Uzbekistan na baadhi ya nchi za Asia ambazo zimechukua misheni muhimu katika huduma ya usalama ya Serikali ya al-Jolani. Magaidi hawa wamechangia katika kusababisha umwagaji damu nchini Syria katika siku zilizopita.
Muundo mpya wa usalama wa Syria unatumia magaidi wenye mwelekeo wa kiakili (za kigaidi) za al-Jolani; Suala hili litasababisha machafuko hatari katika siku zijazo kwa sababu magaidi hawa wameonyesha tabia ya kiholela na ya kikatili hapo awali.
Your Comment