16 Machi 2025 - 17:53
Source: Parstoday
Iran yazindua Jukwaa la Kitaifa la AI: Hatua kubwa kuelekea kwenye kilele cha teknolojia

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua Jukwaa lake la Kitaifa la Akili Mnemba (AI), lililoundwa na watafiti 100 wa Iran, ikiwa ni ishara ya hatua kubwa katika harakati za nchi hii za kujiendeleza na kujitosheleza kiteknolojia.

Kutokana na muhimu wa Akili Mnemba (AI) katika mageuzi ya kidijitali na tasnia ya viwanda vya hali ya juu, jukwaa hilo linaimarisha uchumi unaotegemea maarifa na uwezo wa kiusalama wa Iran. Pia litapunguza utegemezi kwenye majukwaa ya kigeni ya Akili Mnemba na kuzidisha utaalamu wa kiteknolojia wa ndani.

Mkurugenzi wa mradi huo, Mohammad-Reza Hormozi Nejad amesema kuwa Iran inashuhudia hatua kubwa ambayo haijawahi kushuhudiwa hapa nchini katika uga wa teknolojia ya Akili Mnemba.

Jukwaa hili litatoa zana za kukokotoa na ufikiaji wa data kwa watafiti na biashara. Vilevile linawezesha uundaji wa miundo ya kiasili na ya ndani ya AI, ili kupunguza utegemezi kwenye majukwaa ya kigeni.

Jukwaa hili pia lina miundombinu mikubwa ya usindikaji wa data, hifadhidata za mafunzo, na mifano ya AI iliyofunzwa mapema.

Wataalamu wanasema, kwa kuzingatia changamoto zilizopo katika kufikia majukwaa ya hali ya juu ya AI ya kigeni, Jukwaa la Kitaifa la AI la Iran linawakilisha hatua ya kimkakati kuelekea kujitawala kiteknolojia na usalama wa data. Mbali ya kuwezesha utafiti, jukwaa hilo pia linachochea uvumbuzi na ukuaji wa uchumi, na kudhamini nafasi ya Iran katika upeo wa kimataifa wa AI.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha