Nielsen ameeleza hayo mbele ya waandishi wa habari na kusisitiza: "simameni nasi na elezeni bayana kwamba Greenland haiuzwi na haitauzwa katu. Greenland inaendeshwa na watu wa Greenland na hilo halitabadilika kamwe”.
Raia wapatao 1,000 wa Greenland waliandamana siku ya Jumamosi katika mji mkuu Nuuk, wakipinga matamshi yaliyotolewa hivi majuzi ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu uhuru wa nchi yao.
Viongozi wa vyama vya Demokraatit, Naleraq, Inuit Ataqatigiit, Siumut na Atassut walisema katika taarifa ya pamoja kwamba tabia ya Trump "haikubaliki."
Siku ya Alkhamisi iliyopita, rais huyo wa Marekani alihoji na kutilia shaka mamlaka ya utawala ya Denmark juu ya kisiwa hicho na akasema: "Denmark iko mbali sana na haina uhusiano nacho wowote. Ni nini kilichotokea? Kuna mashua ilifika hapo miaka 200 au na ushei. Wanasema wana haki nacho, sijui kama hiyo ni kweli. Kwa kweli sidhani kama ni hivyo.”
Trump aliongeza kwamba, amekuwa akiwasiliana na Denmark na Greenland, na akasema: "inatupasa tufanye kitu" ili kukipata kisiwa hicho.../
342/
Your Comment