Esmail Baqaei Hamaneh ameeleza kuwa: Kwa sasa ujumbe huu haujachapishwa kwenye vyombo vya habari, na kile ambacho kinaenezwa na vyombo vya habari ni uvumi. Baqaei amebainisha haya katika mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari hapa Tehran akifafanua kuhusu barua ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa Iran.
Akijibu swali kwamba Marekani imebua madai na vitisho kuhusiana na Iran baada ya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Yemen, Baqaei Hamaneh amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itajibu vikali uvamizi wowote dhidi ya umoja wa ardhi yake, usalama na maslahi ya taifa la Iran, na hakuna shaka kuhusiana na hilo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Mashambulizi ya kijeshi ya Marekani dhidi ya Yemen bila shaka yoyote ni jinai ya kivita na yanalaaniwa. Amesema, mashambulizi hayo yametekelezwa kinyume na kanuni na taratibu zote za hati ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.
Katika mkutano huo wa kila wiki na waandishi wa habari, Esmail Baqaei Hamaneh ameashiria kuhusu uhusiano wa Iran na Uturuki na kusema: Nchi zote mbili zinafahamu umuhimu wa kudumisha na kupanua uhusiano kati ya pande mbili; hitilafu zilizopo kuhusu masuala ya kikanda ikiwemo suala la Syria kati ya Iran na Uturuki zinashughulikiwa kwa njia ya mazungumzo na maelewano na hakuna hata moja katika pande hizi iliyo tayari kuacha uhusiano wa ujirani mwema uliopo baina ya nchi hizi mbili jirani za Kiislamu na kuathiriwa na ushawishi wa masuala mengine au chambuzi zisizofaa.
342/
Your Comment