Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa kukata misaada na kuvuruga mipango ya kimataifa ya UKIMWI kunaweza peke yake kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo kwa "zaidi ya watu milioni 10 na vifo vya watu milioni tatu."
Adhanom ametoa wito kwa Marekani kufikiria tena msaada wake kwa afya ya ulimwengu.
Baada ya kurejea White House mwezi Januari mwaka huu, Rais wa Marekani, Donald Trump, alisitisha ufadhili wa kifedha kwa taasisi zinazofanya kazi katika nyanja ya kimataifa.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani ameonya kuwa kukatwa ufadhili kwa nchi mbalimbali, ambao hutolewa kupitia mashirika kama vile Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC), kutakuwa na madhara makubwa.
Adhanom ameongeza kuwa jambo hilo litaathiri pakubwa mapambano ya muda mrefu dhidi ya magonjwa kama vile UKIMWI na polio.
342/
Your Comment