Katika ujumbe wake huo aliotoa leo Alkhamisi kwa mnasaba wa kuwadia Mwaka Mpya na Nouruzi ya 1404 Hijria, Pezeshkian amesema: "katika kuanza mzunguko mpya wa masiku, tutaifanya qadari yetu iwe bora zaidi, ya juu zaidi, na ya heshima zaidi kuliko tuliyokuwa nayo na tumeazimia kwa mshikamano wetu na kwa kuwa kwetu kitu kimoja, na kwa imani na itikadi tuliyonayo, na kwa irada na azma yenu nyinyi wananchi tuisafishe Iran na kila machafu, maovu na utovu wa haki na uadilifu; na hatutaacha kufanya kila juhudi ili kulifikia lengo hilo".
Rais Pezeshkian ametoa mkono wa baraka kwa kuwadia Mwaka Mpya na Nouruzi na kusaidifiana na Lailatul-Qadri, kwa Wairani wote ndani na nje ya nchi, kila mahali ulimwenguni, kwa majirani wote na kwa watu eneo lote linalosherehekea Nouruzi, na kuwatakia waishi kwa amani, urafiki na furaha.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu daima amekuwa akishajiisha na kuunga mkono uwekezaji na ushiriki mkubwa zaidi wa wananchi na sekta halisi binafsi katika uchumi, na ametilia mkazo suala hilo muhimu katika utoaji jina la mwaka mpya.
Dakta Pezeshkian ameongeza kuwa, "ili kufikia malengo matukufu na dira adhimu iliyoainishwa na Kiongozi wa Mapinduzi, taifa la Iran linahitaji kubadilika kimtazamo, kuwa na umoja na mshikamano wa ndani, kujiepusha na migawanyiko ya kuwa mirengo kadhaa; na bila shaka suala la kuwa na uhusiano mzuri katika nyanja zote na nchi jirani ndio kipaumbele chetu cha kwanza, na kisha na nchi zote za dunia; na tunalopigania ni kujenga ulimwengu uliojaa amani, udugu na utu na uliojiweka mbali na vitisho, mauaji ya halaiki na mauaji ya kinyama yanayofanywa na watenda jinai na madhalimu; na ili kufikia lengo hili, katika muda wote wa siku za mwaka mpya tutafanya juhudi ili daima tubaki kuwa katika upya.../
342/
Your Comment