20 Machi 2025 - 17:35
Source: Parstoday
Israel yaua watu wengine 71 katika mashambulizi dhidi ya Gaza na kuikalia tena Netzarim

Ripoti zinaonyesha kuwa ndani ya saa 24 zilizopita wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 71 katika miji ya Beit Lahiya, Rafah na Khan Yunis, huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Mauaji haya yamejiri wakati wanajeshi wa Israel wameukalia tena "Ukanda wa Netzarim leo Alhamisi; na hivyo kwa mara nyingine tena kulitenganisha eneo la kaskazini la Gaza na sehemu nyingine za ukanda huo.

Takwimu mpya za Wizara ya Afya ya Palestina zinaonyesha kuwa Wapalestina 49,547 wameuliwa shahidi na 112,719 wamejeruhiwa tangu Israel ianzishe vita na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza. Jumanne wiki hii Israel ilianzisha tena mauaji ya kimbari na mashambulizi ya kinyama dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza baada ya utawala huo kutupilia mbali kwa upande mmoja makubaliano ya kusitisha mapigano iliyoyafikia na harakati ya Hamas. 

Katika muda wa siku tatu zilizopita wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina zaidi ya 500; theluthi mbili wakiwa ni wanawane na watoto. 

Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha watu wa familia mbalimbali wakiuliwa kinyama, huku video nyingi zikiwaonyesha pia watoto wachanga waliouawa na wanajeshi wa Israel.

Kwa mujibu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kuwahami Watoto wa Palestina, watoto wa Kipalestina wapatao 183 waliuawa shahidi na Israel tarehe 18 mwezi huu wa Machi.

Israel imeshadidisha mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza huku hali ya mvutano ikipamba moto pia miongoni mwa walowezi wa utawala huo haramu. 

Huko Quds mashariki inayokaliwa kwa mabavu, maelfu ya walowezi wa Israel wameandamana mitaani wakiitaka serikali kujikita katika suala la kuachiwa huru mateka wakisisitiza kuwa kuendelea vita kutayaweka maisha yao katika hatari kubwa. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha