22 Machi 2025 - 14:34
Wapalestina 130 Wameuawa Shahidi Katika Saa 48 Zilizopita

Katika saa 48 zilizopita, Mashahidi 130 na Majeruhi 263 wamehamishiwa katika Hospitali za Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) -ABNA-, Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa Mashahidi 130 na Majeruhi 263 walihamishiwa katika Hospitali za Ukanda wa Gaza katika muda wa saa 48 zilizopita.

Wizara ya Afya imetoa taarifa (leo hii) siku ya Jumamosi na kubainisha kuwa kutokana na kuuawa Shahidi watu hao, idadi ya Mashahidi wa Kipalestina imefikia 634 na waliojeruhiwa kufikia 1172 tangu Machi 18.

Wizara hii imeongeza idadi ya wahanga wa vita vya mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Gaza kutoka Oktoba 7, 2023 hadi kufikia Mashahidi 49,747 na 113,213 waliojeruhiwa.

Wakati huo huo, idadi kubwa ya wahasiriwa bado wako chini ya vifusi au kwenye barabara, na timu za uokoaji haziwezi kuwafikia.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha