23 Machi 2025 - 16:47
Kuhifadhi Utukufu wa Ramadhani na kuimarisha matumaini, ni sababu ya Nguvu na Ukaribu wa Kiislamu

Ayatollah Hosseini, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Iraq na mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi ameashiria taathira za funga kiutamaduni na kijamii na kusisitiza juu ya ulazima wa kuhifadhi utukufu wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika jamii.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (AS) -Abna-, Ayatollah Hosseini, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu nchini Iraq na Mjumbe wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi, katika mazungumzo yake na Shirika la Habari la Abna, ameashiria athari za Kitamaduni na Kijamii za funga katika jamii za Kiislamu na kusisitiza haja ya kuuhifadhi utukufu wa Mwezi wa Ramadhani na kueleza: Saumu sio tu ni ibada ya mtu binafsi, lakini ina athari pana kwa hali ya kijamii na kitamaduni ya jamii za Kiislamu. Wakati wa mchana, mfungaji hujisikia kama mgeni wa Mwenyezi Mungu, na hisia hii ya utakatifu na wajibu huimarisha hali ya kiroho katika jamii. Ikiwa hali ya jumla ya jamii itaathiriwa na hali ya kiroho ya Ramadhani, hii itasababisha kuongezeka kwa uwajibikaji na heshima kwa maadili ya kidini.

Haja ya Kuhifadhi Utukufu wa Ramadhani Katika Jamii

Akikosoa kutofuatwa kwa Ramadhani katika baadhi ya maeneo ya umma, alisema: Wale ambao ni wasafiri na hawafungi, wamesamehewa katika mtazamo wa Sharia. Lakini wale ambao hawafungi bila ya udhuru wa kidini na kula na kunywa hadharani, kitendo hiki ni kinyume cha kuheshimu anga ya kiroho ya jamii. Kwa bahati mbaya, katika baadhi ya maeneo ya Ziara na Maduka ya vyakula, tunaona utoaji wa chakula kwa umma wakati wa mchana, ambao unachukuliwa kuwa ni kutoheshimu Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Hata wakati wa utawala wa Twaghuti, maduka ya vyakula kama vile chelokabab na migahawa ima vilifungwa au kuendeshwa kwa kuweka mapazia ili umma wa watu usiondolewe kwenye Utukufu wa Ramadhani.

Akiashiria nafasi ya saumu katika mafungamano ya jamii za Kiislamu, Ayatollah Hosseini ameongeza kuwa: Iwapo nchi za Kiislamu zinaweza kutambulisha utamaduni wa saumu na hali ya kiroho ya Ramadhani kimataifa, jambo hilo litapelekea kuongezeka moyo wa matumaini na mafungamano miongoni mwa Waislamu wa dunia nzima.

Kujua mila zinazohusiana na Mwezi wa Ramadhani katika nchi tofauti kama vile Iran, Iraqi, Afghanistan, Syria, Lebanon na hata nchi za Magharibi kutaimarisha mafungamano ya kiroho baina ya Waislamu.

Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu nchini Iraq akisisitiza umuhimu wa kuzingatiwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani amesema: Hali ya anga ya umma ya nchi haipaswi kuwa hivyo kiasi kwamba inakuja chini ya swali na ukosoaji wa Waislamu wengine.Kudumisha hadhi ya kitaifa, heshima ya kidini na hasa heshima kwa Madhehebu ya Ahlul-Bayt (AS) ni jambo la lazima ambalo lazima lizingatiwe. Huu ndio utakuwa msingi wa kuongeza hamasa, matumaini na mafungamano katika jamii ya Kiislamu.

Suluhu za vitendo ili kuimarisha matumaini na kuongeza ushiriki wa vijana katika maendeleo ya nchi

Ayatollah Hosseini, Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu wa Iraq ameashiria ulazima wa kuimarishwa matumaini na nafasi ya vijana katika maendeleo ya nchi na akasisitiza juu ya kupatiwa ufumbuzi wa kivitendo ili kuongeza moyo wa matumaini baina ya wananchi na akasema: Moja ya njia kuu za kuimarisha matumaini katika jamii ni kueleza ukweli wa maendeleo ya nchi. Kwa bahati mbaya, baadhi ya watu kwa kukashifu na kusingizia ubaya, wanasingizia kuwa nchi haijapiga hatua na matatizo yote yanachangiwa na mfumo.Mtazamo huu sio wa haki; Kwa sababu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepata maendeleo makubwa katika nyanja mbalimbali za kisayansi, kiteknolojia, kijeshi na kisiasa na hivi leo inahesabiwa kuwa ni nguvu yenye taathira katika ngazi ya kimataifa.

Akizungumzia mwingiliano (ukaribu) na nchi mbalimbali, aliongeza: Watu na viongozi wengi katika nchi mbalimbali wameshangazwa na maendeleo ya Iran na kuyashangaa mafanikio hayo. Bila shaka, matatizo ya kiuchumi, hasa katika uwanja wa thamani ya fedha za kitaifa, ni hatua dhaifu ambayo suluhisho lazima litolewe. Lakini matatizo haya yasifanye mafanikio ya nchi kupuuzwa.

Ayatollah Hosseini amesisitiza kuwa: Kuimarisha imani na kujitolea kwa Mwenyezi Mungu kuna dhima yenye matokeo katika kuongeza matumaini katika jamii. Mtu anayemwamini Mungu na kumtumaini Yeye, anategemea uwezo wa Mungu usio na kikomo na anasonga kwenye njia ya uzima kwa matumaini. Ikiwa vijana watashikamana na imani na tumaini katika Mungu, hawatakatishwa tamaa wanapokabili matatizo.

Akikosoa kauli mbaya na kashfa dhidi ya viongozi alisema: Kwa bahati mbaya baadhi ya watu hudhoofisha imani ya umma na kuongeza hali ya kukata tamaa katika jamii kwa kukashifu na kueneza habari zisizo na nyaraka (vithibitisho). Kama vile kusengenyana kumeharamishwa katika Uislamu, kusengenyana juu ya viongozi, hasa ikiwa ni uwongo, ni dhambi kubwa zaidi; Kwa sababu hii inasababisha viongozi kupoteza hamasa na ari yao, na watu kutoamini mfumo.

Ayatollah Hosseini aliendelea: Iwapo mtu anafahamu kuhusu ukiukwaji au kushindwa kwa afisa, atoe taarifa kwa taasisi za kisheria na mamlaka husika ili jambo hilo liweze kushughulikiwa. Lakini kuchapisha masuala kama haya bila uthibitisho na katika ngazi ya jamii kutasababisha kukata tamaa na kukatishwa tamaa.

Haja ya kuepuka hukumu za haraka na mtazamo wa kuona mabaya tu

Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu nchini Iraq amebainisha: Moja ya matatizo ya jamii ya leo hii ni kukithiri kwa kukata tamaa (kuwa na mitizamo ya kuona mabaya tu na kupelekea waishi kwa kukata tamaa) na kutoa hukumu za haraka.

Katika Hadithi za Kiislamu, inasisitizwa kwamba tabia za wengine zinapaswa kutendewa mema maadamu hakuna ushahidi wa wazi juu ya ubaya wake. Utamaduni huu ukiwekwa katika jamii, kutoelewana na mabishano mengi yataepukwa.

Aliongeza: Kukata tamaa na uamuzi mbaya huhimiza watu kufanya ukiukaji. Lakini ikiwa watu watatathmini tabia ya wengine kwa msingi wa nia njema, mazingira ya jamii yataelekea kwenye uaminifu na ushirikiano.

Akizungumzia nafasi ya watu katika matukio ya kijamii, Ayatollah Hosseini alisema: Licha ya matatizo ya kiuchumi na mashinikizo ya kimataifa, Taifa la Iran limeonyesha kuwa liko imara katika kuunga mkono fikra za Mapinduzi ya Kiislamu.

Ushiriki mkubwa wa watu katika matembezi ya Siku ya Quds, ni kumbukumbu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu na uungaji mkono kwa wananchi madhulumu wa Palestina, Lebanon na Syria, unaonyesha kina cha imani na mshikamano wa kitaifa. 

Mwishoni, alisisitiza: Ili kuimarisha matumaini na kuongeza ushiriki wa vijana katika maendeleo ya nchi, ukweli wa maendeleo ya Iran lazima usemwe kwa usahihi.

Kuimarisha imani, kupiga vita kauli mbaya na kashfa, kukuza utamaduni wa nia njema na uwepo hai katika matukio ya kijamii ni miongoni mwa njia muhimu zaidi za kufikia lengo hili.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha