27 Machi 2025 - 16:42
Amani ya Palestina, ni Amani ya Tanzania

Wito wa kujitokeza kwa watu wote, Waislamu na Watanzania wote wapenda Haki katika siku ya Kimataifa ya Quds, ili kuungana na Wapalestina katika kutetea Haki zao za Kibinadamu katika Taifa lao la Palestina, na vile yakiwa ni Matembezi ya Masjid Al_Aqsa, ambayo ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt a.s) -ABNA-:  Wito wa kushiriki katika Matembezi ya Amani Duniani (Siku ya Quds Duniani), iliyotangazwa na kuasisiwa rasmi na Marhumu Imam Ayatollah Sayyid Ruhollah Musavi Khomeini  (R.A) , katika kila Ijumaa ya Mwisho ya kila Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, ili kutetea Haki na Uadilifu kwa wadhulumiwa wa Palestina, umetolewa kwa Waislamu wote na Wananchi wote na watu wote huru na wapenda Haki wa Tanzania, ili wajitokeze kwa wingi ili kuungana na Wapalestina katika kutetea Haki zao za Kibinadamu katika Taifa lao la Palestina, na vile yakiwa ni Matembezi ya Masjid Al_Aqsa, ambayo ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu.

Amani ya Palestina, ni Amani ya Tanzania

Matembezi haya ya Amani yatafanyika Siku ya Ijumaa, 28 Machi, 2025 (Ijumaa ya Mwsiho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan - 1446Hijria), kuanzia Saa: 2:30 Asubuhi. Na yataanzia Ilala, Boma, hadi katika Viwanja vya Pipo, Kigogo, Post, Dar-es-salaam - Tanzania.

Amani ya Palestina, ni Amani ya Tanzania

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha