Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la IRGC, Admeli Alireza Tangsiri ametoa matamshi makali kuhusiana na mkao wa kujihami wa Iran na kusisitiza kwamba shambulio lolote dhidi ya Iran litakabiliwa na jibu la uhakika.
Tangsiri amepinga kabisa uwezekano wowote wa Iran kushiriki katika mazungumzo juu ya silaha zake za makombora au msaada kwa makundi ya Muqawama. Amesisitiza kuwa, "Iran kamwe haitajadiliana kuhusu makombora yake au uwezo wa mrengo wa Muqawama."
Amefafanua kuwa, Iran inafuatilia kuwa na uhusiano wa amani na majirani zake, akisisitiza kuwa Tehran kamwe si tishio kwa mataifa mengine ya kieneo.
"Siku zote tunanyoosha mkono wa urafiki kwa nchi za ukanda huu. Sisi Waislamu, hatuna tishio lolote kwa nchi jirani," amesisitiza.
Huku akieleza kuwa Iran haina nia ya kuanzisha vita, Tangsiri amesisitiza kuwa shambulio lolote dhidi ya maslahi ya Iran au watu wake litakabiliwa na jibu thabiti.
Anasisitiza kuwa, "Hatutafuti vita na hatutaki vita. Hata hivyo, ikiwa adui atajaribu kudhuru maslahi yetu au kushambulia watu wetu, lazima wajue kwamba tutajibu."
342/
Your Comment