30 Machi 2025 - 17:36
Source: Parstoday
Wanachuo 300 wapokonywa viza US kwa kuiunga mkono Palestina

Marekani imebatilisha viza za wanafunzi zaidi ya 300 wa kigeni kwa kuratibu na kushiriki katika maandamano ya kuwanga mkono na kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina katika mabewa ya vyuo vikuu kote nchini humo.

Wimbi la kukamatwa na kufukuzwa nchini humo ni sehemu ya juhudi za serikali ya Rais Donald Trump za kukandamiza upinzani dhidi ya jeshi la Marekani na uungaji mkono wa kidiplomasia kwa Israel, ambao umeshika kasi wakati huu ambapo mauaji ya kimbari yanaendelea huko Gaza.

"Tunafanya hivyo kila siku. Kila ninapompata mmoja wa vichaa hawa, ninawanyang'anya viza," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio alisema hayo karibuni.

Rubio alisema viza za wanafunzi zinatolewa kwa madhumuni ya masomo, sio uanaharakati, akisisitiza kuwa, "Tulikupa viza ili uje kusoma na kupata cheti cha digrii, sio kuwa mwanaharakati wa kijamii, na kuharibu mabewa yetu ya vyuo vikuu."

Hatua ya serikali ya Marekani ya kuwatia mbaroni wanaharakati na wanafunzi wa kigeni wanaopinga vita na wanaounga mkono Palestina imezidisha wasiwasi kuhusu kushadidi makabiliano ya kiusalama na watetezi wa Wapalestina na vuguvugu la wanafunzi nchini Marekani.

Wanachuo 300 wapokonywa viza US kwa kuiunga mkono Palestina

Wizara ya Mambo ya Nje na maafisa wa kibalozi nchini humo wametakiwa wafanye mapitio ya mitandao ya kijamii kwa waombaji viza ili kubaini uhusiano wowote na "ugaidi," na uchunguzi maalum kwa wale waliohusika katika maandamano dhidi ya vita huko Gaza. 

Mbinyo na vitendo hivi vya mamlaka za Marekani vimekabiliwa na malalamiko ndani ya vyuo vya Marekani, na vilevile katika duru za kisiasa za nchi hiyo na hata nje ya nchi.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha