30 Machi 2025 - 17:38
Source: Parstoday
China: Tuko tayari kustawisha uhusiano wa kijeshi na Iran na Russia

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China amezungumzia mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyofanywa na majeshi ya Wanamaji ya nchi hiyo, Iran na Russia na kusisitiza kuwa Beijing iko tayari kustawisha ushirikiano wa kijeshi na nchi hizo mbili.

Wu Qian amesema, hadi sasa China, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia zimefanya kwa mafanikio luteka tano za pamoja za majeshi ya wanamaji tangu mwaka 2019 na akaongezea kwa kusema: "Beijing iko tayari kutoa mchango wake katika kudhamini amani na utulivu katika ngazi ya kimataifa na kikanda".Mazoezi ya saba ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la "Ukanda wa Usalama wa Bahari 2025" yalifanyika katika bandari ya kimkakati ya Chabahar ya Iran kuanzia Jumatatu ya tarehe 10 Machi na kuendelea kwa muda wa siku tano kwa kushirikisha vikosi vya wanamaji vya Iran, Russia, na China.

Katika miaka michache iliyopita, China, Russia, na Iran zimefanya mazoezi kadhaa ya kijeshi ya vikosi vya wanamaji sambamba na kuimarisha uhusiano wao wa kimkakati.

Mbali na zana zake zingine za kijeshi, China ilituma katika eneo la luteka ya pamoja na Iran na Russia, manowari yake ya mashambulizi iitwayo Baotou, ambayo ndiyo manowari yenye nguvu zaidi ya kuangamiza makombora ya nchi hiyo.Iran kwa upande wake, ilitumia katika mazoezi hayo ya kijeshi zaidi ya aina 10 za manowari, ikiwa ni pamoja na manowari za kushambulia za Jamaran na Alvand, manowari ya Shahid Bahman Bagheri, na manowari yake mpya kabisa ya kubebea ndege zisizo na rubani.

Nalo jeshi la wanamaji la Russia lilishirikisha katika mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi ya nchi tatu manowari mbili za kushambulia na moja ya lojistiki.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha