Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo katika mahojiano maalumu na shirika la habari la FARS na huku akiashiri kuendelea mashambulizi ya kikatili ya Israel dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Ghaza, amevitaja vitendo hivyo kuwa ni jinai zisizo na kifani katika historia ya binadamu na ameutaka Ulimwengu wa Kiislamu kuchukua hatua za haraka na za uhakika kuwaokoa wanadamu wa Ghaza.
Amezungumzia mauaji ya makumi ya maelfu ya wanawake na watoto wa Palestina na kulazimishwa kuhama idadi kubwa ya watu huko Ghaza na kusema: "Jinai na uhalifu huu wa kutisha haujawahi kushuhudiwa. Mauaji ya maelfu ya wanawake na watoto wasio na hatia yanaendelea, zaidi ya watu laki moja wameshajeruhiwa, makazi na maeneo yao yote yameangamizwa... Qur'ani Tukufu inauelezea Umma wa Kiislamu kuwa ni sawa na mwili mmoja. Hadithi pia zinasisitiza kwamba lazima mtu umsaidie ndugu yako anayedhulumu ili aache kudhulumu na anayedhulumiwa ili ajikomboe. Mafundisho haya yanalifanya suala la kuwasaidia ndugu zetu Wapalestina kuwa ni wajibu wetu wa kidini."
Aidha amekosoa utepetevu wa taasisi za kimataifa katika kuzuia jinai za Wazayuni na kuongeza kuwa: Umoja wa Mataifa umeshindwa kuzuia jinai hizo. Wanadamu wanahitaji kuwa na taasisi mpya na huru itakayoweza kusaidia mataifa ya dunia hasa mataifa yanayokandamizwa kama Palestina.
342/
Your Comment