Mwandishi wa Radio Tehran amemnukuu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi akisema hayo katika kikao kilichohudhuriwa na kundi la wasomi na wanaharakati wa kiutamaduni na vyombo vya habari wa Algeria kujadili uhusiano wa Tehran na Algiers.
Katika mkutano huo, Araghchi ameelezea misimamo ya kimisingi ya Iran katika masuala mbalimbali ya sera za kigeni, likiwemo suala la kuunga mkono Muqawama na haki ya wananchi wa Palestina ya kupambania mustakbali wao na kadhia ya nyuklia ya Iran.
Akizungumzia uvamizi wa miaka themanini wa ardhi ya Palestina na mpango wa kikoloni wa kuwaangamiza kabisa wananchi wa Palestina, ambao umeendelea kwa muda wa miezi 17 sasa kwa mauaji ya kikatili ya umati katika jinai ambayo haijawahi kushuhudiwa huko Ghaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan sambamba na mashambulizi ya kikatili yanayoendelea kufanywa na Israel huko Lebanon na Syria, pamoja na mashambulizi ya kichokozi ya Marekani nchini Yemen, Waziri wa mambo ya Nje wa Iran amesema: tajiriba na uzoefu wa miongo minane iliyopita unaonesha kwamba hakuna njia nyingine isipokuwa Muqawama na kusimama kidete kupambana na utawala ghasibu wa Israel.
342/
Your Comment