Ayatullah Kazem Seddiqi amebainisha hayo katika khutba zake za Sala ya Ijumaa ya leo ya hapa mjini Tehran na kusisitiza kwa kusema: "Ninakuusieni enyi waja wa Mwenyezi Mungu na ninaiusia nafasi kumcha Mwenyezi Mungu. Kumcha Allah ni daraja la juu kabisa la uchamungu... Mtu anapodumisha ukuruba na kunong'ona na Mola wake, Allah humpa heshima mtu huyo."
Katika sehemu nyingine ya khutba zake, Imam wa Sala ya Ijumaa ya Tehran amegusia mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja baina ya Iran na Marekani yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi kwa upatanishi wa Oman mjini Muscat na kusema kuwa, katika mazungumzo ni lazima mtu awe na imani kwamba upande mwingine utatekeleza kile unachoahidi. Tusisahau kuwa ni rais huyu huyu wa Marekani ndiye aliyechana mapatano ya nyuklia ya JCPOA.
Ayatullah Seddiqi aidha amesema: "Marekani ina uadui usioweza kusuluhishwa na Iran na dhidi ya Uislamu na imani na itikadi zetu bali na taifa letu lote ambalo hivi sasa limesababishiwa majeraha makubwa na Marekani ambayo hayawezi kupona."
Akizungumzia vikwazo na athari zake kwa uchumi wa ndani, amesema: "Mpango wa Kiongozi Muadhamu wa kuwa na uchumi wa Muqawama, umetuchorea mstari ulio wazi kwamba tunapaswa kutatua matatizo yetu kwa kutegemea uwezo wetu wa ndani ya nchi bila ya kuhitaji misaada kutoka nje. Maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia tuliyopata Iran katika kipindi kifupi tu ni makubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani kwa kutegemea uwezo wetu wa ndani, na Mwenyezi Mungu akipenda, matatizo yaliyopo kwenye njia ya kuimarisha uchumi pia yatatatuliwa kwa dhamira na uvumilivu.
Amesema Iran haiogopi kufanya mazungumzo na kwamba mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yamekuwepo muda mrefu tu.
342/
Your Comment