Katika ujumbe wake huo kwenye mtandao wa kijamii wa X, Esmail Baghaei amesema: "Kwa nia njema na umakini kamili, tunaipa diplomasia fursa ya kweli. Marekani inapaswa kuthamini uamuzi wetu huu huu ambao tumeuchukua licha ya kuendelea Marekani kutoa maneno yao ya kiuadui dhidi yetu."
Aidha ameandika: "Tumeamua tusihukumu mambo mapema au kutabiri tu; Tumeamua kutathmini kivitendo nia na ukweli wa upande mwingine siku ya Jumamosi ili baadaye tuangalie tuchukue hatua gani."
tarehe 9 Aprili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi alitangaza kuanzishwa tena mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington mjini Muscat Oman.
Aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X-Net kwamba: "Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani yataanza Jumamosi (Aprili 13) nchini Oman."
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesema kuwa, Iran na Marekani zitakutana nchini Oman siku ya Jumamosi kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika ngazi ya maafisa wa ngazi za juu.
Alisisitiza kuwa hii ni fursa na pia ni mtihani, na mpira uko katika uwanja wa Marekani.
342/
Your Comment