"Kuendelea vitisho vya nje na kuiweka Iran katika hali ya shambulio la kijeshi kunaweza kufuatiwa na hatua za kujihami kama vile kufukuzwa wakaguzi wa IAEA na kusitishwa ushirikiano nayo," ameandika Ali Shamkhani katika ujumbe uliochapishwa kwenye jukwaa la kijamii la X, jana Alkhamisi.
Shamkhani ameendelea kusema: "Kuhamisha mada zilizorutubishwa na kupelekwa maeneo salama ambayo hayajatangazwa nchini Iran pia kunaweza kuwa kwenye ajenda."
Matamshi hayo yametolewa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukariri tena vitisho vya uwezekano wa kutumia hatua za kijeshi ikiwa Tehran haitafikia makubaliano na Washington kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye malengo ya kiraia.
Siku kadhaa zilizopita pia Rais Masoud Pezeshkian wa Iran alisisitizia msimamo usiotetereka wa Tehran wa kutoanzisha vita na nchi yoyote na wakati huo huo akasema Iran iko imara kwa ajili ya kujihami. Aliongeza kuwa: "Tumeshauthibitishia ulimwengu kuwa hatutaki vita, hatutaki bomu la nyuklia na hatutaki machafuko. Hivi sasa ni zamu ya Wamarekani kuthibitisha kivitendo kuwa kweli wanataka mazungumzo.
342/
Your Comment