Mwaka huu wa 2025, Israel imedhinisha bajeti kubwa zaidi ya ulinzi katika historia yake, zaidi ya dola bilioni 30. Ni bajeti kubwa hasa kwa ajili ya kupanua vita. Wakati huo huo, mazungumzo ya kusitisha mapigano yalisitishwa kwa njia ya kustaajabisha. Kwa nini? Kwa sababu Israel iliweka sharti jipya la upande mmoja mezani, ambalo kwa hakika liliua kabisa mazungumzo na kuyafanya yapoteze maana. Nini kilitokea baadaye?
Katika usiku mmoja tu baada ya mazungumzo kuvunjika, mashambulizi ya anga ya Israel yaliua zaidi ya watu 400 katika Ukanda wa Gaza. Nukta ya kuashiriwa zaidi ni kwamba: Ikulu ya White House ilithibitisha kuwa operesheni hiyo imefanyika kwa kuratibiwa na Merekani!
Swali linalojitokeza hapa ni kwamba: Je, ukatili wote huu ni kwa ajili ya kujitetea? Au kwa lengo la kuiokoa serikali ya Netanyahu isiporomoke na kuanguka? Au la, pengine ni kwa ajili ya kutumia akiba ya silaha za zamani zilizorundikwa kwknye maghala na kununua silaha mpya?
Baadhi ya uchunguzi wa maoni wa zaidi ya 70% ya washiriki unasema kwamba, iwapo vita vitasimama na uchaguzi ukafanyika, Netanyahu atashindwa. Kwa hivyo vita ni fursa kwake. Ni fursa ya kubakia madarakani.... Na bila shaka, vita vya Gaza pia ni fursa ya dhahabu kwa makampuni ya silaha kwa ajili ya kuuza zana nyingi zaidi.
Sasa hebu twende Marekani...
Nyaraka zinaonyesha kuwa operesheni za hivi majuzi za Marekani nchini Yemen zimeenda sambamba na kuanza tena vita vya Gaza. Hii ni licha ya kwamba, katika kipindi cha kusitishwa mapigano huko Gaza, wapiganaji wa harakati ya Houthi nchini Yemen hawakufanya hata shambulia moja dhidi ya meli zinazoiunga mkono Israel.
Wakati huo huo, Trump, ambaye anajaribu, kama alivyodai, kufufua uchumi wa Marekani na kuweka uhai mpya katika sekta ya uzalishaji nchini kwake, ametumia mbinu ya zamani ya kuanzisha vita ili kutia uhai mpya katika gurudumu la sekta ya viwanda. Naam, anachochea vita ili kupandisha juu hisa za makampuni ya kutengeneza silaha ya Marekani, ambayo uchumi wao unakula na kunywa na kubakia hai kutokana na vita. Kwa njia hii, Trump pia anayasaidia makampuni ya kijeshi ambayo yalifadhili kampeni zake za uchaguzi wa rais, na kwa maneno mengine, analipa fadhila!
Nukta muhimu ya kuashiria hapa ni kwamba, kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, jumla ya mapato yaliyotokana na mauzo ya silaha yalifikia rekodi ya dola bilioni 318.7 mwaka jana 2024 pekee, ikiwa ni ongezeko la 29% ikilinganishwa na mwaka wa kabla yake.
Lakini pia hatupaswi kusahau jambo moja:
Trump na Netanyahu wana kitu kinachowakutanisha pamoja, nacho ni utegemezi wa moja kwa moja kwa lobi na makundi ya mashinikizo na yenye ushawishi ya tasnia ya viwanda vya zana za kijeshi.
Nafupisha yote yaliyosemwa kwa maneno kadhaa:
Netanyahu analinda kiti chake cha madaraka kwa kuendeleza vita.
Trump anaimarisha uwezo wake wa kifedha kwa kuuza silaha zaidi.
Na makampuni na lobi za kutengeneza silaha za Marekani pia zinapata faida ya mabilioni ya dola...
342/
Your Comment