15 Aprili 2025 - 22:08
Source: Parstoday
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wajadili mazungumzo ya Oman

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudi Arabia wamefanya mazungumzo ya simu na kujadiliana kuhusu uhusiano wa pande mbili na maendeleo ya kikanda na kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia, Faisal bin Farhan walifanya mazungumzo kwa njia ya simu siku ya Jumatatu, ambapo Araghchi amemtaarifu bin Farhan kuhusu mazungumzo ya Jamhuri ya Kiislamu na Iran huko mjini Muscat na misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu maendeleo ya kieneo na kimataifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemweleza Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia kuhusu mazungumzo ya hivi karibuni yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani mjini Muscat na duru inayofuata ya mazungumzo hayo, ambayo, kama duru ya kwanza, yataandaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman mjini Muscat.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia ameshukuru kwa maelezo aliyopewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kuhusiana na suala hilo na kukaribisha mchakato wa mazungumzo hayo.

Sayyid Abbas Araghchi, ambaye aliongoza mazungumzo na mwakilishi wa Marekani Steve Witkoff yaliyofanyika mjini Muscat, Oman, Jumamosi iliyopita, ameelezea matumaini yake kuwa mazungumzo hayo yataleta matokeo yanayohitajika kwa Iran na eneo zima.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Saudia wajadili mazungumzo ya Oman

Wakati huo huo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, amepuuzilia mbali uvumi kuhusu mahali patakapofanyika duru ya pili ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani.

"Baada ya mashauriano, imeamuliwa kuwa Muscat (mji mkuu wa Oman) itaendelea kuandaa duru ya pili ya mazungumzo haya, ambayo yatafanyika Jumamosi," Baghaei alisema jana Jumatatu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha