21 Aprili 2025 - 22:55
Source: Parstoday
Katika ujumbe wa Pasaka: Papa atoa wito wa kusitishwa mapigano huko Gaza

Katika ujumbe wake wa Pasaka, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kwa mara nyingine tena ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Ujumbe wa Pasaka wa Papa Francis, amesomwa na msaidizi wake, katika mwonekano wa muda mfupi kwenye balcony ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, licha ya udhaifu wa kimwili uliotokana na maradhi ya nimonia.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani, ambaye amekuwa akieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya Wapalestina wanaoishi Gaza, ameitaja hali ya eneo hilo la Palestina kuwa ya kuhuzunisha na kusikitisha.

Papa ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano ili kuachiliwa huru wafungwa wa Kizayuni na kuwasaidia watu wenye njaa wa Gaza, akisema: "Tangazeni usitishaji vita, waachieni mateka na wasaidieni watu wanaokabiliwa na njaa."

Madaktari wameshauri kupunguzwa shughuli za Papa Francis wakati huu akipata nafuu kutokana na nimonia.

Msimamo huo wa Papa unakuja wakati mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati ukiendelea na jamii ya kimataifa ikitafuta suluhisho la kumaliza mizozo hiyo. 

Katika ujumbe wa Pasaka: Papa atoa wito wa kusitishwa mapigano huko Gaza

Zaidi ya Wapalestina elfu 50 wameuawa shahidi katika kampeni ya mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina hasa katika eneo la Ukanda wa Gaza.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha