Katika mahojiano hayo aliyofanyiwa siku ya Jumapili, Grossi amesema: "pande zote mbili ziko tayari kujadili vipengele vya uhakika".
Mkurugenzi Mkuu huyo wa IAEA ameongezea kwa kusema, hadi hapa yalipofikia, ameridhishwa na mchakato wa mazungumzo na akafafanua kwa kusema: "mazungumzo haya yangeweza kuvunjika katika duru ya pili, na kwa hiyo, kila kitu kingeweza kusita".
Bila kutoa ufafanuzi alisema: "kulikuwepo na hatari. Lakini badala yake, anga iliyotawala Rome inaonyeshwa kuwa upo uwezekano wa kupigwa hatua".
Makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 yaliyojulikana kama JCPOA, ambayo Iran iliyafikia na Marekani, Russia, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani yalifungua njia ya kupunguzwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu kwa sharti la Tehran nayo kukubali kupunguza kwa kiwango kikubwa urutubishaji wa madini ya urani na kuacha kuweka akiba ya urani yake iliyorutubishwa.
Hata hivyo wakati Donald Trump alipoingia madarakani katika muhula wake wa kwanza wa urais mwaka 2018, alitangaza kujitoa Marekani katika makubaliano hayo na kuweka vikwazo vikali dhidi ya Iran. Kufuatia hatua hiyo ya Marekani, Iran nayo ikatangaza kuanza tena kurutubisha madini ya urani kwa ajili ya mpango wake wa nyuklia.
Hivi sasa Trump anataka anataka kufikia makubaliano mengine mapya ya nyuklia na Tehran.../
342/
Your Comment