21 Aprili 2025 - 22:58
Source: Parstoday
Mipango na malengo makubwa ya Iran kwa ajili ya kushirikiana na nchi za Kiafrika

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeratibu mipango na kuainisha malengo yake kwa ajili ya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi na bara la Afrika.

Katika miaka ya karibuni, Iran imeratibu mipango ya kuimarisha ushirikiano na nchi za bara hilo kwa kuzingatia uwezo wake wa kiuchumi na ule wa nchi za Kiafrika. Vikao vya pande mbili na viongozi wa Kiafrika na maonyesho mbalimbali ni miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na pande mbili kwa shabaha ya kuimarisha ushirikiano kati ya Iran na nchi za Kiafrika. 

Kuwepo kwa maliasili nyingi kumelifanya bara la Afrika lizingatiwa kiuchumi duniani, huku nchi zilizoendelea kiviwanda na makampuni ya kimataifa yakitaka kuwekeza haraka iwezekanavyo na kufaidika na utajiri mkubwa wa bara hilo.

Katika uga wa kisiasa, kuimarisha uhusiano na nchi za Kiafrika pia ni muhimu kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Wakati huo huo zipo nchi 30 za Kiislamu katika bara la Afrika, na takriban asilimia 50 ya wakazi wake ni Waislamu, jambo ambalo pia ni muhimu kiutamaduni kwa Iran.

Sayyid Rasul Mohajir, Naibu Mkuu wa Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema wafanyabishara na maafisa wa kiuchumi kutoka nchi 126 duniani wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika. Sayyid Rasul ameeleza kuwa: Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Iran na Afrika utafanyika mjini Isfahan na wageni wa mkutano huo watakaguua uwezo wa kiuchumi na kiviwanda wa mji huo.

Bara la Afrika, mbali na kuwa na utajiri mkubwa wa maliasili na kuwa mshirika mzuri wa Iran kiuchumi, katika upande wa kisiasa pia linaweza kuwa na mchango katika kuiunga mkono Iran katika asasi za kieneo na kimataifa, jambo ambalo linaweza kufikiwa kwa kuzingatia masuala ya pamoja ya pande hizo mbili.

Iran pia ikiwa ni nchi yenye nguvu katika kanda ya Magharibi mwa Asia, kwa kuwa  na miundombinu ya usafirishaji wa reli na barabara pamoja na bandari muhimu za kibiashara katika Ghuba ya Uajemi, inaweza kuwa njia ya mawaisliano kati ya nchi za Kiafrika na nchi za Asia ya Kati, Caucasus na Russia kwa ajili ya kuuza bidhaa nyingi za kilimo za nchi hizo. 

Kuzinduliwa safari za usafirishaji wa meli, kutayarisha miundombinu, kuongeza ubadilishanaji wa bidhaa na kutia saini makubaliano ya kupunguza ushuru wa kibiashara kunaweza pia kuwa na athari katika kuzidisha biashara kati ya Iran na bara la Afrika. 

Mkutano wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Afrika ni kielelezo cha azma kubwa ya maafisa wa kidiplomasia na kiuchumi wa Iran katika kuendeleza uhusiano na nchi za Kiafrika. 

Mipango na malengo makubwa ya Iran kwa ajili ya kushirikiana na nchi za Kiafrika

Wakati huo huo kuendelea mikutano ya kiuchumi na kufanyika mazungumzo zaidi kutaandaa uwanja wa kustawisha uhusiano wa pande mbili, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatoa kipaumbele maalumu kwa bara la Afrika katika kuendeleza sera zake za msingi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na nchi huru na zinazojitawala.

Uwezo wa kisayansi na kiuchumi wa Iran utakuwa na taathira chanya katika kupanua uhusiano na nchi za Kiafrika, na wakati huo huo uwepo wa makampuni ya Iran katika bara la Afrika utarahisisha kazi ya kustawisha uhusiano wa kiuchumi na nchi za bara hilo.

Viongozi wa Afrika pia katika miaka ya karibuni wameonyesha hamu kubwa ya kuimarisha ushirikiano na Iran katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kisiasa, na suhula na uwezo wa kiuchumi wa Iran katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya nishati na maarifa unaweza kuwa msingi mzuri kwa ajili ya ushirikiano wa pande mbili. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha