Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen, Nasr al-Din Amer, ametoa matamshi hayo Jumanne, siku moja baada ya mtawala huyo wa Israel kuapa kujibu mashambulizi yanayoendelea ya Yemen dhidi ya ngome za Israel.
Jeshi la Yemen, tangu Oktoba 2023, limefanya mamia ya mashambulizi kama hayo, kama jibu kwa vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendeshwa na utawala wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.
Mashambulizi hayo yamelenga hasa meli za utawala haramu wa Israel na meli zinazosafirisha bidhaa kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, na hivyo kulazimisha meli hizo kuzunguka Afrika ili kufika katika bandari zinazokaliwa na utawala huo. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa bei za bidhaa kwa walowezi wa Kizayuni na kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wa utawala haramu wa Israel. Amer amesema: “Netanyahu ni adui yetu, na daima tunajitahidi kuwafanya maadui zetu wakasirike.”
Amer amesisitiza kuwa: “Kuwasaidia watu wa Palestina ni ombi la watu wa Yemen,” akieleza jinsi raia wa Yemen wanavyoandamana kila wiki kwa maelfu kwa ajili ya kuunga mkono Palestina, wakitoa wito kwa nchi yao kuongeza msaada wake kwa ajili ya kufanikisha lengo la ukombozi wa Palestina.
Amer, ambaye pia ni mkuu wa Shirika Rasmi la Habari la Yemen, Saba, alimwelezea Netanyahu kama mhalifu wa kivita, akirejelea hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya waziri mkuu huyo wa Israel mwaka jana, kutokana na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza.
Afisa huyo amesema Netanyahu anapaswa kufikishwa mahakamani badala ya kutoa vitisho. Aidha, amebainisha tofauti kubwa kati ya matendo ya utawala wa Kizayuni na majibu ya jumuiya ya kimataifa, akisema, “Kimya dhidi ya uhalifu wa utawala wa Kizayuni kunachochea utawala huo kuendeleza uhalifu zaidi.”
342/
Your Comment