Kwa mujibu wa taarifa ya Dkt. Munir Al-Bursh, Mkurugenzi Mkuu wa Afya wa Gaza, tangu Oktoba 7 2023 wakati jeshi la utawala haramu wa Israel lilipoanzisha mauaji ya kimbari dhidi ya Ukanda wa Gaza, watoto wapatao 17,954 na wanawake 12,365 wameuawa shahidi.
Al-Bursh ameeleza kuwa vikosi vya Kizayuni kwa makusudi vinashambulia maeneo ya raia na makambi ya wakimbizi wa ndani. Ameongeza kuwa zaidi ya watoto 52 wamepoteza maisha kutokana na utapiamlo, na 17 wengine kutokana na baridi kali isiyovumilika. Wakati huo huo, amesema katika Ukanda wa Gaza kuna wagonjwa 22,000 wanaohitaji matibabu ya haraka, kati yao 13,000 wako katika hali mahututi.
Katika sekta ya afya, hali imeelezwa kuwa mbaya mno, huku hospitali 20 zikiwa zimefungwa kabisa na hospitali 18 zikifanya kazi kwa masharti magumu kutokana na uhaba mkubwa wa vifaa na dawa.
Aidha, Al-Bursh amefichua kuwa zaidi ya 1,400 ya watumishi wa afya wameuawa, na wengine takribani 360, akiwemo Dkt. Hossam Abu Safiyeh, wamejeruhiwa. Amesema kuwa mfumo wa afya wa Gaza sasa uko kwenye hatua ya karibu kabisa ya kusambaratika kabisa.
Al-Bursh amebanisha masikitiko na malalmiko makubwa kutokan na ukimya wa ajabu wa jumuiya za kimataifa kuhusu hali ya Gaza, akisisitiza hitaji la haraka la hatua za dharura za kuokoa sekta ya afya ya Ukanda wa Gaza.
342/
Your Comment