25 Aprili 2025 - 22:43
Source: Parstoday
Pigo la Yemen kwa Wall Street; Hisa za silaha za Marekani zaporomoka

Viwanda vya kutengeza silaha vya Marekani vimezidi kupata hasara kutokana na Yemen kufunga Bahari Nyekundu isitumiwe na meli za Marekani, za Israel na chombo chochote cha baharini kinachoupelekea vitu utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la Fars limechapisha makala ya kiuchambuzi kuhusu pigo inalopata Marekani kutokana na Jeshi la Yemen kufunga Bahari Nyekundu na kuandika; Kupungua kwa kiasi kikubwa thamani ya hisa ya makampuni makubwa ya silaha ya Marekani wiki hii kumevutia hisia za wachambuzi wengi wa mambo. Kuporomoka hisa hizo za makampuni ya silaha ya Marekani kunatokana pia na hatua ya Jeshi la Yemen kupiga marufuku meli za Marekani zisitumie Bahari Nyekundu na hilo ni pigo jingine kwa uchumi wa dola la kibeberu la Marekani.

Sababu nyingine iliyotajwa na mwandishi wa makala hiyo ni vita vya kibiashara vilivyoanzishwa na Marekani dhidi ya China na dunia kiujumla chini ya kaulimbiu ya Trump ya "Marekani Kwanza." 

Kwa upande wake gazeti la Financial Times limeripoti kuwa vita vya kibiashara vya Donald Trump dhidi ya China na nchi nyingine vimepunguza mauzo ya nje ya bidhaa za Marekani na kuongeza gharama za uzalishaji kutokana na kupanda bei malighafi.

Aidha kufungwa Bahari Nyekundu na kutoweza meli za Marekani kutumia bahari hiyo kumesababisha usumbufu katika usambazaji wa bidhaa za Marekani na ndio maana hisa ya makampuni ya silaha ya Marekani imeporomoka.

Serikali ya Yemen imesema kuwa, haitozifungulia njia meli za Marekani, Israel na zote zinazoelekea kwa utawala wa Kizayuni hadi pale Tel Aviv itakapokomesha jinai zake huko Ghaza Palestina na kuacha kuuzingira ukanda huo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha