1 Mei 2025 - 23:47
Source: Parstoday
Asasi za kimataifa: Maghala ya chakula Gaza yamebakia tupu

Asasi mbalimbali za kimataifa zimeonya kuhusiana na hali mbaya ya uhaba na ukosefu wa chakula katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, hivi sasa maghala ya chakula katika ukanda huo yapo tupu.

Mashirika ya kimataifa hayo ya yametangaza kuwa, chakula chote katika Ukanda wa Gaza kimeisha, na kueleza kwamba, maafa ya kibinadamu katika Ukanda huo yamefikia kiwango cha maafa na sasa eneo hilo liko katika hatua ya njaa halisi.

Tahadhari za kimataifa kuhusu kushadidi njaa na mgogoro wa njaa katika Ukanda wa Gaza zinaendelea kukua katika kivuli cha mzingiro wa kila upande wa Ukanda huo kwa muda wa miezi miwili iliyopita, sambamba na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika Ukanda wa Gaza.

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifaa umetangaza kuwa, eneo la Ukanda wa Gaza litakabiliwa na hali mbaya zaidi ya kibinadamu katika siku za usoni na kwamba, kuna haja ya kuchukuliwa hatua kuzuia kutokea hilo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, baraza la mawaziri la Israel limeidhinisha mswada wa kupiga marufuku kuingizwa misaada yoyote ya kibinadamu huko Ghaza licha ya kwamba Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu yameonya kuwa wananchi wa Gaza wamo kwenye mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha vita vya kikatili vya pande zote dhidi ya ukanda huo, mwezi Oktoba 2023.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha