Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: binti mmoja kutoka nchini Australia ambaye alijiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh, alikamatwa na kupigwa mpaka kufa alipotaka kutoroka katika kikundi hicho cha kigaidi.
Kwamujibu wa ripoti hii, mabinti wawili kutoka nchini Australia mwaka uliopita walitoroka nyumbani kwao na kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh kiliopo nchini Syria katika wilaya ya Al-Raqqah nchini humo.
Mmoja kati ya mabinti hao amesema: Samra Kesinovic ambaye ni binti wa miaka 18 ameuwawa kwa kosa la kufanya juhudi za kutaka kutoroka katika kikundi hicho cha kigaidi na kumkamata hatimaye kupigwa mpaka akuwawa.
Kesinovic na rafiki yake kipenzi Sabina Selimovic wa miaka 15 mwaka 2014 walikwenda Vienna baadaye kwenda chini Syria kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Daesh, huku wakiwa na lengo la kuwa wanandoa wa jiadi ya kikundi hicho, hivyo baada ya muda kadhaa walifanikiwa kufunga ndoa na vijana wawili wa kikundi hicho cha kigaidi.
Mabinti hao wawili kutoka Australia mara nyingi walikuwa wakionekana katika kurasa za mitandao ya kigaidi wakiwa wamevaa baibui na kufunga nikabu (kininja) huku wakiwa wameshika bunduki ya Kalashnikov mkononi.
Mabinti hao wawili ni kati ya wengi wasiohisabika ambao walijiunga na kikundi hicho cha kigaidi kisichokuwa na huruma nchini Iraq na Syria kwa malengo yasiokuwa na mashiko na potovu.
mwisho wa Habari/290