8 Januari 2016 - 14:18
Gaidi wa Daesh amnyonga mama yake nchini Syria

Mmoja kati ya wanachama wa Daesh nchini Syria amuuwa mama yake mzazi mbele ya mjumuiko wa watu nchini humo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha Daesh chahusika kwa mara nyingine na mauaji ya kusikitisha nchini Syria, kwamba kikundi hicho cha kigaidi kimemnyonga mwanamke aliekuwa akiitwa Lina Kasimu aliye na umri wa miaka 45 kwa sababu kuwa yeye ni mfuasi wa madhehebu ya Alawiy, mama huyo pia alikuwa ni mfanyakazi wa idara ya posta nchini humo.
Ama suala la kusitisha zaidi katika mauaji hayo ni kwamba aliyemnyoga mwanamke huyo ni kijana aliye na jina la Ali Saqar mtoto wa mwanamke huyo wa madhehebu ya Alawiy, huku mtoto huyo alimyonga mama yake huku akidai kuwa anaitumikia dola ya kiislamu ya Daesh.
Kikundi cha kigaidid cha Daesh kinaitakidi kuwa wafuasi wa madhehebu ya Alawi wa Syria kuwa ni wameritadi na hukumu yao ni kunyogwa popote watakapo kamatwa.
mwisho wa Habari/290