Umoja wa Mataifa umesema hatua hiyo inahatarisha maisha ya mamilioni ya watu kote ulimwenguni.
Januari mwaka huu, Umoja wa Mataifa uliwasilisha ombi la dola bilioni 2.4 ili kuwasaidia watu milioni 10.5 katika nchi ya Yemen iliyoharibiwa na vita, huku ikikadiria kuwa watu milioni 19.5 ndio wanaohitaji msaada.
Katika wiki za hivi karibuni, mabadiliko sawa na hayo yalitangazwa pia katika mataifa ya Ukraine na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, takriban watu milioni 67.4 wa eneo la Pembe ya Afrika hawana uhakika wa chakula. Hayo yametangazwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki (IGAD).
Kati ya watu milioni 67.4, milioni 38 wanaishi kwenye nchi wanachama wa IGAD zikiwemo Djibouti, Ethiopia, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Uganda. Wengine wako katika nchi nyingine zinazounda Pembe ya Afrika yaani Jamhuri ya Afrika ya Kati na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambayo ina eneo kubwa la ardhi linalofika hadi katikati mwa Afrika.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imebainisha kuwa, majanga ya mara kwa mara ya hali ya hewa na migogoro inazidisha umaskini na uhaba mkubwa wa chakula na utapiamlo katika eneo la Pembe ya Afrika.
342/
Your Comment