28 Mei 2025 - 20:11
Source: Parstoday
Araghchi: Iran inalaani jaribio lolote la kuharibu umoja wa Waislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inalaani vikali jaribio lolote la kuharibu umoja na mshikamano wa Waislamu hususan wakati huu wa anga ya kiroho na kimaanawi ya Msimu wa Hija.

Sayyid Abbas Araghchi ameashiria sera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kupigania umoja na mshikamano katika safu za Waislamu na kusisitiza kuwa, Waislamu wanapaswa kuzidisha umoja na mshikamano wao na kujiepushe na hatua zozote za kuharibu umoja wao hasa wakati huu wa ibada za Hija na anga ya kiroho na kimaanawi inayotawala wakati huo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika hivi kwenye mtandao wa kijamii wa X: "Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali jaribio lolote la kuharibu umoja wa Waislamu, hasa katika anga ya kimaanawi ya Msimu wa Hija."

Sayyid Araghchi pia ameandika: "Tumetia nia ya kweli na isiyotetereka ya kutoruhusu mtu yeyote kuharibu uhusiano wetu wa kidugu na majirani zetu, ikiwa ni pamoja na jitihada zinazozidi kuzaa matunda za kuimarisha uhusiano wetu na Saudi Arabia."

Vilevile ameeleza kuwa "Iran inathamini sana usimamizi mzuri na wa kuridhisha wa Hija ya mwaka huu."

Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake huo kwenye mtandao wa kijamii wa X, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameandika: "Pamoja na salamu shukrani kwa serikali na watu wa Saudi Arabia katika kuwakaribisha mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Allah, ninawatakia mafanikio katika kuendelea na njia hii."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha