Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, gazeti la Israel Hayom limetangaza katika ripoti yake kwamba Wazayuni ambao wamekosa makazi kutokana na kuharibiwa majengo yao wanapata shida hata ya kupata dawa zao.
Katika mahojiano na Israel Hayom, Wazayuni hao wamesema: "Tulilazimika kukimbia makazi yetu huko Ramat Gan kutokana na ukali na nguvu ya mashambulizi ya makombora ya Iran, lakini taasisi husika za Israel hazijali matatizo yetu na hazitilii maanani hata kidogo."
Mmoja wa Wazayuni hao amesema: "Nyumba yangu imeharibiwa kabisa, walitwambia kwamba watatupa makazi mapya, walitakiwa kutupigia simu lakini hakuna mtu aliyetupigia simu, hatuna pa kwenda, ilibidi niende nyumbani kwa mwanangu usiku, lakini nyumba yake ni ndogo sana na hakuna uwezekano wa mimi kuishi huko, hawakunipa hata dawa yangu. Simu yangu ya mkononi nayo haina MB."
Mzayuni mwingine amesema, kwa bahati nzuri mama yangu alikuwa nasi wakati wa shambulio la makombora la Iran. Tangu tulipoona kwenye TV eneo hili limeharibiwa, tumekuwa tukipiga simu lakini hakuna anayetujibu.
Mkazi mwingine wa Ramat Gan amesema, walitujulisha kwamba watatupigia simu, lakini hadi leo hakuna mtu aliyenipigia simu.
Habari hiyo imetangazwa huku utawala wa Kizayuni ukiwa umeweka pingamizi kali sana la vyombo vya habari visiripoti kabisa vituo vya kijeshi na taasisi nyingine muhimu zilizopigwa kwa makombora ya Iran.
Kuhusiana na hilo, mwandishi wa gazeti la Haaretz pia amekosoa uzembe wa mawaziri wa Israel kwenye ukurasa wake wa X akisema, "Nimetembelea maeneo mawili yaliyopigwa na makombora ya Iran katika muda wa saa 24 zilizopita. Uharibifu huo haufikiriki, lakini jambo la kushangaza ni kwamba hakuna waziri aliyetembelea maeneo hayo hadi sasa. Sijaona mbunge yeyote wa Knesset wote wamejificha katika mashimo yao kama panya."
342/
Your Comment