Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Sala ya Ijumaa imeswaliwa Leo hii katika Kituo cha uwakilishi wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s.a.w.w) nchini Malawi Khatibu akiwa: Ustadh Abdulrashid Shuaib.
Katika Khutba yake, alizungumzia umuhimu wa Siku ya Ghadir katika historia ya Uislamu, akieleza vipengele vyake vya kiitikadi na kijamii, pamoja na nafasi yake katika kuimarisha dhana ya Uwilaya katika Uislamu.
Sheikh Abdurashid Shuaib alisisitiza juu ya haja ya kuihuisha siku hii tukufu na kueneza uelewa wake miongoni mwa Waislamu, kwa kuwa ina mchango mkubwa katika kuimarisha umoja na uaminifu kwa njia ya Ujumbe wa Kiislamu.
Your Comment