15 Juni 2025 - 13:22
Source: Parstoday
Iran yaangusha ndege ya tatu ya kivita aina ya F-35, marubani wawili Waisraeli wakamatwa

Jeshi la Iran (Artesh) limeripoti kuangusha ndege ya tatu ya kivita aina ya F-35 inayomilikiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel, kwa kutumia mifumo ya ulinzi wa anga iliyotengenezwa ndani ya Iran.

Kwa mujibu wa tamko rasmi la Jeshi, rubani wa ndege hiyo ya kisasa kabisa iliyoundwa Marekani alinaswa akiwa hai baada ya kujirusha kwa parachuti katika maeneo ya magharibi mwa Iran.

Kwa tukio hili la karibuni, Iran sasa imefanikiwa kuangusha jumla ya ndege tatu za kivita za F-35 tangu Israel ilipoanzisha hujuma zake siku ya Ijumaa. Kati ya ndege mbili zilizoangushwa awali, imedokezwa kuwa rubani mmoja aliuawa papo hapo, huku mwingine akikamatwa na vikosi vya Iran. 

Vita kati ya Iran na Israel vimechacha kufuatia mauaji ya takribani raia 100, maafisa wa kijeshi, na wanasayansi wa nyuklia wa Kiirani, waliouawa shahidi katika mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya makazi ya raia mjini Tehran. Wakati wa kuanzisha uchokozi huo, Israel ililenga maeneo nyeti ya nyuklia pamoja na kambi kadhaa za kijeshi kote nchini Iran.

Iran, kwa upande wake, imetoa jibu kali kwa mawimbi matano ya makombora ya masafa marefu kuelekea Israel, na kusababisha uharibifu mkubwa katika zaidi ya vituo 150 vya kijeshi na ujasusi ndani ya ardhi hiyo inayokaliwa kwa mabavu. Kwa sasa, Iran inaendeleza mashambulizi kwa kutumia droni za kujitoa mhanga (Kamikaze), huku duru za kijeshi zikidokeza kuwa mashambulizi makali zaidi kwa makombora yanatarajiwa kufuata ndani ya saa chache zijazo.

Ndege za kivita aina ya F-35 zinazotumiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel  zinatambuliwa kama za kisasa zaidi.  F-35 imeundwa na kampuni ya anga ya Lockheed Martin ya Marekani. Jeshi katili la Israel ni miongoni mwa majeshi machache duniani yaliyopewa ruhusa rasmi na Marekani kutumia ndege hii ya kizazi cha tano yenye teknolojia ya hali ya juu ya kuepuka rada. Pamoja na uwezo huo wote wa kukwepa rada, Jeshi la Iran limeweza kuitungua kwa kutumia makombora yaliyoundwa nchini na hivyo kuifanya Iran kuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kuangisha ndege hii ya kisasa ya F-35

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha