Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi la Yemen limetoa taarifa na kuonya kuwa iwapo Marekani itashiriki kijeshi katika mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meli za kibiashara na Meli za kivita za Marekani katika Bahari Nyekundu zitashambuliwa.
Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji rasmi wa jeshi la Yemen:
"Shambulio lolote la pamoja la Marekani na Israel dhidi ya Iran ni uchokozi wa moja kwa moja dhidi ya Umma wa Kiislamu na litakuwa na shabaha ya kuupa udhibiti Utawala wa Kizayuni katika eneo hili la Kikanda na kuyapokonya uhuru wa mataifa mengine"
"Yemen haitasalia kuishia kutizama na kutojali uchokozi wowote dhidi ya nchi ya Kiislamu."
Your Comment