Huku viwango vya utapiamlo vinavyoongezeka maradufu miongoni mwa watoto na ugavi wa maziwa ya watoto wachanga ukipungua kwa kiwangi cha kutisha, mzozo wa kibinadamu huko Gaza unazidi kuongezeka, na kuweka maelfu ya maisha hatarini.
Habari zaidi zinasema kuwa, familia tofauti katika Ukanda wa Gaza zinaripotiwa kuhatarisha maisha yao ili tu kupata chakula cha siku. Kauli ya OCHA inathibitisha madhara makubwa ya kuendelea kuzuiwa kwa misaada kwa raia wa Gaza.
Haya yanaripotiwa siku chache baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada kwa Ajili ya Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kutangaza kwamba, Ukanda wa Gaza unasumbuliwa na hali mbaya na kwamba njaa imekithiri katika eneo hilo, na watu wanazimia barabarani kutokana na njaa kali.
UNRWA ilitahadharisha Ijumaa kwa mara nyingine kuhusu hali ya mgogoro wa binadamu katika Ukanda wa Gaza na uhaba mkubwa bidhaa za chakula.
Inaelezwa kuwa, mfumo wa kusambaza misaada wa sasa huko Gaza unaamiliana kinyume na ubinadamu na familia zenye njaa na hofu, zilizojeruhia na zilizochoka za Wapalestina.
Shirika la UNRWA limeeleza kuwa kuna mgogoro mkubwa wa njaa na ukosefu wa chakula katika Ukanda wa Gaza na kwamba wakazi wa eneo hilo wanazimia mitaani kutokana na njaa inayoongezeka.
Your Comment