1 Oktoba 2025 - 13:12
Trump Aishitaki "Wall Street Journal" na Rupert Murdoch kwa "Kuchafua Jina Lake"; Aomba Fidia ya Dola Bilioni 10

Gazeti la Wall Street Journal lilidai kuwa mwaka 2003, Trump alimtumia Jeffrey Epstein barua yenye maudhui ya kingono pamoja na picha ya uchi kwa kumbukumbu ya kutimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Mashitaka hayo yameibuliwa kufuatia taarifa iliyochapishwa na gazeti la Wall Street Journal iliyodai kuwa mwaka 2003, Trump alimtumia Jeffrey Epstein barua yenye maudhui ya kingono pamoja na picha ya uchi kwa kumbukumbu ya kutimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake.

Trump ameyaita madai hayo kuwa ni "uongo, ya kuharibu heshima na yenye kuchafua jina", akisisitiza kuwa hajawahi kuandika barua kama hiyo wala kutengeneza picha kama hiyo.

Kufuatia kesi hiyo, msemaji wa kampuni ya Dow Jones amesema kuwa ripoti ya Wall Street Journal iliandaliwa kwa kutegemea vyanzo vya kuaminika, na watatetea usahihi na ukweli wa habari hiyo.

Your Comment

You are replying to: .
captcha