25 Desemba 2025 - 13:15
Ujumbe wa Hongera wa Rais Pezeshkian kwa Kiongozi wa Wakatoliki Duniani

Katika kuendeleza diplomasia ya kidini na kuimarisha maadili ya kuishi kwa amani kati ya wafuasi wa dini mbalimbali, Rais wa Jamhuri alitoa ujumbe rasmi wa pongezi kwa kiongozi wa Wakatoliki duniani, akisisitiza umuhimu wa kuheshimiana, mazungumzo ya kidini na mshikamano wa kibinadamu katika dunia ya leo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Rais wa Jamhuri alimtumia Papa Leo wa XIV, Kiongozi wa Wakatoliki duniani, ujumbe wa pongezi kwa mnasaba wa kuadhimishwa kwa kuzaliwa kwa heri kwa Nabii Isa bin Maryam (a.s) na kuanza kwa Mwaka Mpya wa Miladia 2026.

Pongezi hizi ni muendelezo wa diplomasia ya kidini na kuimarisha maadili ya kuishi kwa Amani kati ya wafuasi wa dini mbalimbali. Ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unasisitiza umuhimu wa kuheshimiana, kuwa na mazungumzo ya kidini na mshikamano wa kibinadamu katika dunia ya leo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha