29 Desemba 2025 - 14:38
Mfano wa Somaliland utaenea kwa nchi nyingine / Taa ya kijani kwa hatua hii italigharimu eneo kwa gharama kubwa za kiusalama!

Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Oman, katika mahojiano na ABNA, ameielezea hatua ya Israel ya kuitambua Somaliland kuwa ni jaribio hatari la kulazimisha uhalisia mpya dhidi ya wananchi wa Palestina. Alisisitiza kuwa uamuzi huu si tu ukiukaji wa wazi wa haki za Wapalestina, bali pia unaweza kutathminiwa kuwa sehemu ya mradi wa kuliondoa Gaza wakazi wake na kufanya uhandisi wa idadi ya watu katika eneo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Ofisi ya waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni hivi karibuni imetangaza kuwa Benjamin Netanyahu, waziri mkuu wa utawala huo, ametambua rasmi Somaliland kama nchi huru. Hatua hii imekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Somalia, Uturuki, Misri, Iran na Djibouti, na imeelezwa kuwa ni tishio kwa umoja na mamlaka ya eneo la Somalia.


Katika muktadha huo, Zaher Al-Mahrouqi, mwandishi na mchambuzi wa kisiasa wa Oman, katika mahojiano na ABNA aliitaja hatua hiyo kuwa ni uingiliaji wa wazi katika masuala ya ndani ya nchi nyingine. Alisema kuwa kuitambua kile kinachoitwa Somaliland hakuchangii amani wala utulivu, wala haisaidii kutatua migogoro, bali kunafungua njia ya wimbi jipya la migawanyiko katika ulimwengu wa Kiarabu na bara la Afrika.


Al-Mahrouqi alipinga vikali aina yoyote ya kugawa nchi, akisisitiza kuwa mgawanyiko wa nchi husababisha kuundwa kwa tawala dhaifu na kufungua milango ya kuingilia kati kwa nguvu za kigeni.


Kwa mujibu wa mchambuzi huyo wa Oman, hatua hii inaweza kuunda mfano hatari na hata kusababisha vitendo kama hivyo, ikiwemo uwezekano wa Israel kuitambua Yemen ya Kusini.


Al-Mahrouqi pia alirejelea ripoti zinazoonyesha kuwa utambuzi wa Somaliland unahusishwa na mpango wa kuwahamisha wakazi wa Gaza kwenda katika eneo hilo. Alionya kuwa iwapo ripoti hizo zitathibitika, mpango huo utakuwa ni ukiukaji wa wazi wa haki za Wapalestina na juhudi za kuliondoa Gaza wakazi wake, jambo ambalo linaweza pia kutishia kwa kiwango kikubwa uthabiti wa nchi za Pembe ya Afrika.


Mwisho, Al-Mahrouqi alibainisha upinzani wa serikali ya Somalia pamoja na sehemu ya jamii ya kimataifa dhidi ya uamuzi huu, akisema: utawala wa Kizayuni unaweza kusukuma mbele miradi kama hii tu kwa ridhaa ya kimyakimya ya baadhi ya nchi za Kiarabu, na nchi hizo zitakuja kulipa gharama kubwa sana kwa upande wa usalama wa kitaifa katika siku zijazo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha